📍 Bukavu, DRC – 18 Juni 2025 — Katika hali inayoashiria mabadiliko makubwa kwenye uwanja wa vita, maelfu ya wapiganaji wa kizalendo (Wazalendo) wanaripotiwa kuwa wamewasili na kuimarika kwa wingi katika jiji la Bukavu, wakijipanga kwa ajili ya hatua kali dhidi ya waasi wa M23 na mashirika mengine ya uasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wakazi wa Bukavu wameshuhudia mafuriko ya wapiganaji wa Wazalendo wakipita mitaani, wengine wakishika doria, wengine wakikesha kwenye maeneo muhimu ya mji. “Bazalendo biko mingi sana tena sana Bukavu! Wanatufariji sana wananchi. Vita itapita Bukavu hadi Kigali, Rwanda – kieleweke,” alisema mmoja wa wakazi wa eneo hilo kwa hisia kali.

🔥 AXE ZOTE ZACHUKULIWA NA WAZALENDO

Kwa mujibu wa duru za usalama, njia kuu zote za kimkakati (axe) kuingia na kutoka Bukavu zimeripotiwa kuwa chini ya udhibiti wa Wazalendo. Waasi wa M23 na washirika wao wanaripotiwa kuwa katika hali ya mkanganyiko na kukimbia maeneo mbalimbali ya milima, wakikwepa mashambulizi makali ya kizalendo.

🌍 Dunia Yatambua Ushujaa wa Wazalendo

Matukio haya ya karibuni yameanza kuleta taharuki kimataifa, huku mashirika ya haki za binadamu, vyombo vya habari vya kimataifa, na nchi jirani wakianza kutambua na kushukuru juhudi za wapiganaji wa Wazalendo kwa kujaribu kuokoa DRC dhidi ya uingiliaji wa kigeni na waasi wanaotuhumiwa kusaidiwa na Rwanda.

🗣️ KAULI YA WANANCHI

“Wazalendo si tu wanapigana – wanalinda utu wa Kongo. Hii ni vita ya kizalendo, ya haki, ya kulinda ardhi yetu. Dunia nzima sasa inaanza kuelewa ukweli,” alisema mama mmoja mkazi wa Bagira kwa machozi ya shukrani.

🛑 MecaMedia itaendelea kufuatilia kwa karibu hali hii inayoendelea kubadilika kwa kasi mashariki mwa DRC, hasa hatua za mashujaa wa Wazalendo.

✍️ Mwandishi: MANGWA

📌 #WazalendoDRC #Bukavu #AxeZoteChiniYaUdhibiti #KigaliKieleweke #MasharikiYaDRC #M23 #KongoInaamka #MecaMedia