
Uvira, Alhamisi 12 Juni 2025 – Saa 12:00 jioni, kijana mmoja mwenye umri wa takriban miaka 25 ameuliwa kwa risasi katika mtaa wa Songo, avenue ya Marché, ndani ya komini ya Kalundu.
Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na tukio hilo, kisa kilitokea baada ya kutokea mjadala mkali kati ya marehemu na marafiki zake, wote wakitajwa kuwa wanachama wa kundi la Wazalendo. Chanzo kamili cha ugomvi huo bado hakijafahamika wazi, lakini hali hiyo ilisababisha mmoja wao kutumia silaha ya moto, na kumpiga risasi kijana huyo aliyefariki papo hapo.
Majina ya wahusika na ya marehemu bado hayajafahamika rasmi kwa wakati huu, lakini vyombo vya usalama vimewasili eneo la tukio na kuanza uchunguzi.
Tukio hili limezua taharuki kubwa katika mtaa huo na kuzua maswali kuhusu usalama wa ndani ya makundi ya wenye silaha, pamoja na mahusiano yao binafsi na kijamii.
🔎 Tunafuatilia kwa karibu na tutawapa taarifa kamili mara tu majina yatakapothibitishwa rasmi.
📍 MCMR-RDC – Uvira
✍️ Mwandishi: MANGWA
#Uvira #Kalundu #Wazalendo #HabariZaUsalama #MCMR #DRC #BreakingNews #MECAMEDIA
