Bukavu, Juni 12, 2025 – Habari za kipelelezi kutoka mashuhuda wa tukio la kikatili lililotokea katika eneo la Funu, baada ya mkutano wa Bourgmestre wa Kadutu, zinaonesha kuwa Josué King SAFARI, kijana anayetajwa kuwa mmoja wa viongozi wa kikundi cha waasi cha M23-AFC, ndiye aliyeamuru kupigwa risasi kwa raia wa Kongo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na uchunguzi wa ndani:

  • Josué King SAFARI ni mtoto wa Mchungaji SAFARI Mukombe
  • Ni mwanafunzi wa zamani wa Chuo Kikuu cha HOPE, katika kitivo cha Informatique de gestion, kuanzia mwaka 2011
  • Inadaiwa kuwa tayari ameanza kuomba msamaha kupitia simu, na audios mbili za sauti yake akiomba msamaha zimeshapatikana

Tukio hilo la kutisha limetikisa jamii ya Bukavu na kuzua maswali mengi kuhusu usalama wa raia na namna baadhi ya vijana wa Kongo wanavyogeuka kuwa vibaraka wa vikundi vya kigaidi vinavyodhoofisha nchi yao.

Wito kwa Jamii:

Ujumbe huu ni tahadhari kwa raia wote, hususan wale waliopo ndani na nje ya Kivu Kusini: huyu kijana anayetoka katika jamii yetu amekuwa chombo cha mateso kwa wananchi wake mwenyewe. Ajuwe kuwa picha yake iko katika kumbukumbu za wahusika, na matendo yake hayawezi kufutwa kirahisi.

Kifo cha raia wa Kongo hakiwezi kuwa biashara ya kawaida. Watakao simama kuuwa bila huruma, kwa amri au kwa risasi, watakumbukwa na historia – lakini si kwa wema.

📍 Taarifa rasmi ya MECAMEDIA

✍️ Mwandishi: MANGWA

#Funu #M23AFC #JosueKingSafari #Bukavu #UhalifuWaKivita #MECAMEDIA #JusticePourLesVictimes #DRC

By mangwa