Serikali Yasaini Mkataba wa Kuboresha Reli ya Kisangani-Ubundu

Makamu wa Kwanza wa Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Uchukuzi, Mawasiliano na Ufunguaji wa Maeneo, Jean-Pierre Bemba, ameongoza hafla ya kusaini mkataba muhimu wa ukarabati na uboreshaji wa reli kati ya Kisangani na Ubundu, mkoani Tshopo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hafla hiyo imefanyika Ijumaa, tarehe 4 Julai 2025, jijini Kinshasa, ambapo serikali ya Congo imeingia makubaliano na konsortium ya kampuni ya Korea Kusini KECC na kampuni ya Congo Masco Énergies, kwa msaada wa kifedha kutoka benki ya Equity BCDC.

Kwa mujibu wa mkataba huo, kazi ya ukarabati na uboreshaji wa reli hiyo itaanza ndani ya siku 15 zijazo, na mradi mzima unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36.

Mradi huu ni hatua muhimu katika kufungua mikoa ya Kaskazini-Mashariki mwa Congo na kuongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa na watu kati ya Kisangani na Ubundu, huku pia ukitarajiwa kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi ya eneo hilo.

Mwandishi: MANGWA