
🇨🇩 RTNC Yamsahau Joseph Kabila Katika Orodha ya Marais wa Zamani wa Congo
Katika maadhimisho ya miaka 65 ya uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yaliyofanyika Jumatatu, Juni 30, Radio Télévision nationale congolaise (RTNC) ilirusha matangazo maalum yakiorodhesha marais wote waliowahi kuiongoza nchi hiyo. Hata hivyo, majina yote yalitajwa isipokuwa la rais wa zamani Joseph Kabila Kabange ambaye aliiongoza Congo kwa kipindi cha miaka 18.
Swali kubwa limeibuka: je, ni kosa la kawaida au kufutwa makusudi?
Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema ni vigumu kuamini kuwa ni kosa la bahati mbaya hasa kwa tukio la hadhi kubwa kama maadhimisho ya uhuru wa taifa. Wengine wanaona kuwa huenda ni ishara ya mgawanyiko wa kisiasa au makusudi ya kufuta mchango wa Kabila katika historia ya Congo.
Mpaka sasa RTNC haijatoa maelezo yoyote rasmi juu ya tukio hilo ambalo limezua mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi na wadau wa historia ya nchi hiyo.
✍️ Mwandishi: MANGWA
