
MUSIQUE – HÉRITIER WATA AKAMATWA KISA “MAGODA”!
Msanii maarufu wa muziki wa Congo, Héritier Wata (jina halisi: Héritier Bondongo Kabeya), amekamatwa Jumatano hii tarehe 23 Julai na kufikishwa katika parquet ya Kinshasa/Gombe.
Kukamatwa kwake kunahusiana na malalamiko rasmi juu ya wimbo wake mpya “Zala”, ambao unahusisha miondoko ya kidensi ya “Magoda” iliyotajwa kuwa chafu na isiyofaa kwa jamii, hasa vijana.
Tume ya Kitaifa ya Udhibiti wa Nyimbo na Maonyesho tayari ilikuwa imepiga marufuku video ya wimbo huo kwa maelezo kuwa inakiuka maadili na huenda ikaharibu tabia za vijana.
Kwa sasa, Héritier Wata anazuiliwa katika kituo cha parquet, akisubiri uamuzi wa kisheria kuhusu sakata hilo.
Ituri: Mke wa kiongozi wa kijiji na mtoto wajeruhiwa kwa bomu
