
📍 Bagira, Bukavu – Jumatano, 18 Juni 2025 — Mlio wa risasi umeripotiwa mapema leo katika wilaya ya Bagira, jiji la Bukavu, hali iliyoleta hofu na mtafaruku mkubwa miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.
Mashuhuda wameripoti kwamba milio ya risasi ilianza kusikika tangu alfajiri, na kwa sasa, hali ya taharuki imetanda mitaani. “Ndio, milio ya risasi inasikika hapa Bagira, watoto wameachwa huru kutoka mashuleni… shughuli zote zimesimama hadi sasa,” alisema mmoja wa wakazi wa eneo hilo alipoongea na MecaMedia kwa njia ya simu.
🛑 Shule Zafungwa, Watoto Wakarudishwa Nyumbani
Mamlaka za shule mbalimbali zimeripotiwa kuchukua hatua za haraka kwa kuwafunga wanafunzi na kusitisha masomo kwa siku ya leo, kwa kuzingatia usalama wao. Vilevile, maduka, masoko, na usafiri wa umma vimesimamishwa huku wananchi wakijifungia manyumbani kwao wakihofia usalama wao.
🔍 Chanzo cha Milio ya Risasi Hakijabainika Rasmi
Hadi sasa, hakuna tamko rasmi kutoka kwa maafisa wa jeshi au serikali ya mkoa kuhusu chanzo cha tukio hili. Hata hivyo, hali hiyo imezua maswali mengi miongoni mwa wakazi, hasa ikizingatiwa muktadha wa mvutano wa mara kwa mara mashariki mwa DRC.
➡️ MecaMedia inafuatilia kwa karibu maendeleo ya tukio hili na itawapa taarifa zaidi pindi zitakapopatikana.
✍️ Mwandishi: MANGWA
📌 #Bagira #Bukavu #MilioYaRisasi #TaharukiDRC #UsalamaMashariki #MecaMedia
