
🇨🇩🏆 DRC Yaahirisha Kambi ya CHAN 2024 Kwa Sababu ya Ukosefu wa Fedha
Kinshasa, 17 Julai 2025
Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imepata pigo kubwa kuelekea mashindano ya CHAN 2024, baada ya mazoezi yao kuahirishwa kutokana na matatizo ya kifedha. Maandalizi ya timu hiyo maarufu kama Les Léopards yameingia dosari zikiwa zimesalia siku chache kabla ya michuano kuanza Agosti 2, 2025.
Kocha mkuu Otis Ngoma alikuwa tayari ametangaza kikosi cha wachezaji 36 waliopaswa kuingia kambini kwa siku tano katika hoteli moja jijini Kinshasa. Hata hivyo, mnamo Julai 17, hoteli hiyo ilikataa kuwahudumia chakula cha mchana wachezaji kutokana na deni kubwa lililodaiwa na timu hiyo.
Mashindano ya CHAN (African Nations Championship) yanajumuisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani tu, na mwaka huu yataandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda, na Tanzania, kuanzia 2 hadi 30 Agosti.
Timu ya DRC, ambayo imeshinda CHAN mara mbili tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009, ilitarajiwa kuanza mashindano kwa kishindo kwa kucheza dhidi ya Kenya katika Uwanja wa Kimataifa wa Moi, Nairobi, tarehe 3 Agosti.
Kusitishwa kwa kambi hiyo ni kigezo cha tahadhari kwa mashabiki wa Congo, huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu maandalizi na uwezo wa timu hiyo kushiriki kwa mafanikio kwenye mashindano hayo muhimu ya Afrika.
Doha Yafungua Mlango wa Amani DRC na M23
