DRC na M23 Watia Saini Azimio la Kanuni za Amani Qatar

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kundi la waasi wa M23 wametia saini azimio la kanuni (declaration of principles) siku ya Jumamosi huko Doha, Qatar, hatua muhimu inayolenga kusitisha mapigano ya muda mrefu mashariki mwa DRC.

Kwa mujibu wa taarifa ya APA ikinukuu Al-Arabiya, makubaliano hayo yalifikiwa kati ya wawakilishi wa pande zote mbili katika mji mkuu wa Qatar, Doha.

Kundi la M23 ambalo liliteka maeneo makubwa ya mashariki mwa DRC yenye utajiri wa madini kupitia mashambulizi ya ghafla mwezi Januari na Februari 2025, lilikuwa likisisitiza kupata makubaliano yake ya kusitisha mapigano na serikali ya Kinshasa, hasa baada ya mshirika wao Rwanda kusaini mkataba wa amani na Marekani mwezi uliopita.

Mashariki mwa DRC imekuwa ikikumbwa na mizozo kwa zaidi ya miaka 30, hali iliyoibua janga la kibinadamu huku maelfu ya watu wakilazimika kuyakimbia makazi yao. Katika mashambulizi ya M23 mapema mwaka huu, maelfu walipoteza maisha na miji mikuu ya mikoa ya Goma na Bukavu ikaangukia mikononi mwa waasi.

Ingawa mstari wa mbele wa mapigano umetulia tangu Februari, bado mapigano hukumba maeneo mbalimbali kati ya M23 na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.

Makubaliano haya ya Doha yanachukuliwa kama hatua ya matumaini kuelekea suluhisho la kudumu, huku dunia ikisubiri kuona kama pande husika zitatekeleza kwa vitendo makubaliano hayo.

mecamediaafrica.com

Polepole Asema Hapambani na Serikali Isiyo na Haki – Adai Dada Yake Ametekwa

Kinshasa Yaitaka Uganda Kutoa Maelezo kwa Kufungua Mpaka na M23