Katika kile kinachoonekana kama kupinga uvumi wa kusalimu amri, Bertrand Bisimwa, Naibu Mratibu wa AFC/M23, ametangaza kupitia akaunti yake ya X siku ya Jumatatu, Julai 21, kuwa mazungumzo yanayoendelea mjini Doha kati ya kundi lake na serikali ya DRC hayahusiani na kuondoka kwao nchini, kama ilivyodaiwa na baadhi ya duru.

“Sio katika uwanja wa vita wala kwenye meza ya mazungumzo ambayo tunafanya kazi kuelekea kuondoka kwetu nchini,” aliandika Bisimwa.

Doha Yafungua Mlango wa Amani DRC na M23

Mazungumzo ya Amani ya DRC na M23 Yaendelea Doha

Kwa mujibu wake, lengo la mazungumzo ni kuhakikisha kwamba raia wote wa Kongo wanaweza kuishi kwa amani na hadhi katika nchi yao. Alieleza kuwa hii siyo kujisalimisha bali ni mazungumzo kuhusu utawala, ambao AFC/M23 inautambua kama chanzo kikuu cha mzozo wa mashariki mwa DRC.

Kauli hii inatolewa wakati ambapo dunia inatazamia mafanikio kutoka kwenye mchakato wa amani unaoendelea mjini Doha, ukiratibiwa na Qatar kwa kushirikiana na wadau wa kimataifa.

Wakati hayo yakiendelea, wasiwasi umeibuka kuhusu iwapo makubaliano ya amani yanaweza kufikiwa ikiwa AFC/M23 inaweka wazi kuwa haitajiondoa kutoka maeneo wanayoyadhibiti, hususan Kivu ya Kaskazini na Kusini.

M23 na Rubaya

mecamediaafrica.com