
Urusi Yadai Kuangusha Droni 60 za Ukraine Katika Shambulio la Usiku
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imeripoti kuwa mifumo yao ya ulinzi wa anga imefanikiwa kuharibu na kuzuia jumla ya droni 60 zilizodaiwa kuwa za Ukraine katika shambulio lililotokea usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa, idadi kubwa ya droni hizo zilitunguliwa katika maeneo tofauti ya Urusi na katika maji ya bahari jirani. Taarifa hiyo imeeleza kuwa:
- Droni 17 zilitunguliwa juu ya eneo la Crimea
- Droni 16 zilitunguliwa katika mkoa wa Rostov
- Droni 11 zilidunguliwa juu ya Bahari ya Azov
- Droni 5 zilitunguliwa katika mkoa wa Kursk
- Droni 4 zilitunguliwa katika mkoa wa Saratov
- Droni 3 zilitunguliwa juu ya Bahari Nyeusi
- Droni 2 zilitunguliwa katika mkoa wa Belgorod
- Droni 1 ilitunguliwa katika mkoa wa Voronezh
- Droni 1 ilitunguliwa katika mkoa wa Oryol
Urusi imesisitiza kuwa mashambulizi hayo yamezidi kushika kasi, lakini mifumo yao ya ulinzi wa anga inaendelea kuimarika katika kuzuia vitisho hivyo.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa huru zilizothibitisha madai haya kutoka pande nyingine au mashirika ya kimataifa. Ukraine haijatoa tamko rasmi kuhusiana na tukio hili.
Mgogoro kati ya Urusi na Ukraine unaendelea kuchukua sura mpya kila siku, huku matumizi ya droni yakionekana kuwa sehemu muhimu ya vita hivi vya kisasa.
Habari hii imeandaliwa na MANGWA
