Screenshot

🔴 Mkataba wa Amani Kati ya DRC na Rwanda Kutangazwa Rasmi Ijumaa Hii Washington

Washington, 25 Juni 2025 – Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza rasmi kuwa mkataba wa amani kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Rwanda utasainiwa Ijumaa tarehe 27 Juni 2025 jijini Washington.

Katika tangazo lililotolewa pembeni mwa Mkutano wa Kilele wa NATO, Rais Trump alieleza kuwa makubaliano hayo yatakuwa hatua muhimu kwa uthabiti wa Afrika ya Kati na kwa amani ya dunia.

“Tarehe 27 Juni, mkataba wa amani utasainiwa hapa Washington kati ya DRC na Rwanda. Hii itakuwa hatua kubwa kwa uthabiti wa Afrika ya Kati na kwa amani ya dunia,” alisema Donald Trump, akisisitiza kujihusisha kwake moja kwa moja katika mchakato wa upatanishi huo.

Hadi sasa, mamlaka za Congo na Rwanda bado hazijatoa tamko rasmi kuhusiana na tangazo hili, lakini vyanzo kadhaa vya kidiplomasia vimethibitisha maandalizi ya hafla ya kusaini mkataba huo jijini Washington.

Makubaliano haya yanatarajiwa kumaliza mvutano wa muda mrefu na mapigano ya mara kwa mara mashariki mwa Congo ambayo yamekuwa yakiathiri amani ya eneo hilo kwa zaidi ya miongo mitatu.

Muandishi: MANGWA

#RDC #Rwanda #MkatabaWaAmani #Trump #Washington #HabariZaLeo