Screenshot
Constant Mutamba

Kinshasa, Juni 16, 2025 – Katika kikao cha jioni cha Jumapili tarehe 15 Juni, Bunge la Taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limepitisha ombi la kuanzishwa kwa mashitaka dhidi ya Waziri wa Sheria na Gavana wa Haki, Constant Mutamba, baada ya kura ya maoni yenye matokeo mazito.

Kati ya wabunge 363 waliopiga kura:

✅ Wabunge 322 waliunga mkono mashitaka,

❌ 29 walipinga,

⚖️ 12 walijizuia kupiga kura.

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya uwasilishaji wa ripoti ya kamati maalum ya muda iliyokuwa imekabidhiwa kuchunguza ripoti ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Rufaa, Firmin Monde.

Katika hoja yake, Firmin Monde alisisitiza kuwa: “Ushahidi uliotolewa na Waziri Mutamba haukanushi tuhuma zinazomkabili, bali unathibitisha nia ya wazi ya kuhusika katika ubadhirifu wa mali ya umma.”

Mutamba anadaiwa kuhusika na upotevu wa takribani dola milioni 19 za Kimarekani, ambazo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa gereza jipya mjini Kisangani, mkoani Tshopo.

Hatua hii inaonesha kushamiri kwa mvutano wa wazi baina ya Waziri Mutamba na Mwendesha Mashtaka Mkuu Firmin Monde, ambapo mwelekeo wa sasa unaashiria kuwa upande wa mashtaka umejizatiti vilivyo.

⛓️ Iwapo mashitaka yatathibitishwa rasmi na mahakama, Constant Mutamba atakuwa miongoni mwa maafisa waandamizi wa serikali kufikishwa kizimbani kwa tuhuma za ufisadi katika kipindi cha hivi karibuni.

✍️ Mwandishi: MANGWA

📌 #RDC #Ubadhirifu #Bunge #ConstantMutamba #Kisangani #HabariLeo #MecaMedia

By mangwa