
Uvira, Juni 15, 2025 – Taarifa ya kusikitisha imetokea katika mtaa wa Kavivira, mjini Uvira, ambapo mwanamke mmoja ameuawa kikatili na mume wake baada ya kudaiwa kukutwa akifanya tendo la ndoa na mwanaume mwingine ndani ya nyumba yao.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mwanaume huyo alirejea ghafla kutoka kazini na kuwakuta mke wake akiwa kitandani na mwanaume mwingine. Katika hali ya hasira kali, alichukua silaha ya jadi (panga) na kumjeruhi vibaya mke wake kwa kumkata kichwa na mikono. Mwanamke huyo alifariki dunia papo hapo kutokana na majeraha ya kutisha.
Mwanaume aliyekuwa na mke huyo alifanikiwa kutoroka na hadi sasa hajapatikana. Polisi wa eneo la Uvira wameanza uchunguzi wa kina kuhusu tukio hili la kusikitisha, na juhudi za kumkamata mtuhumiwa wa pili bado zinaendelea.
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi unaendelea na kuhimiza jamii kuripoti mienendo yote inayohatarisha amani ya familia na usalama wa watu.
🔴 Wito kwa jamii:
Matukio ya aina hii yanapaswa kutufunza umuhimu wa mawasiliano, uvumilivu na usuluhishi katika ndoa. Jamii yetu inapaswa kulaani vikali ukatili wa aina hii na kuhakikisha kesi za ndoa zinashughulikiwa kwa njia ya amani na si kwa kumwaga damu.
✍️ Mwandishi: MANGWA
📌 #Uvira #HabariZaUhalifu #JamiiYetutujirekebishe #MECAMEDIA
