Katika tukio la kusikitisha lililotokea mjini Goma, waasi wa kundi la M23, wanaojiita “wakombozi wa watu,” wamefanya uhalifu mwingine wa kivita kwa kuwaua raia wasio na hatia kwa risasi za moja kwa moja katika eneo la Funu.

Kwa mujibu wa mashuhuda walioko karibu na tukio hilo, wapiganaji wa M23 walifyatua risasi kiholela katika maeneo ya makazi, wakiwalenga moja kwa moja raia waliokuwa wakijaribu kuokoa maisha yao. Miili ya baadhi ya waathirika ilionekana kutapakaa kwenye ardhi ya uwanja wa wazi, huku wengine wakijeruhiwa vibaya.

Tukio hili limezua hofu, hasira na masikitiko makubwa kwa wakazi wa Goma na jamii ya kimataifa, likithibitisha tena kuwa madai ya M23 ya kupigania uhuru na haki ni ya kificho, huku wakitekeleza mashambulizi yenye lengo la kuwatisha na kuwanyamazisha wananchi.

🖊 Mwandishi: MANGWA

M23 #Goma #Funu #UhalifuWaKivita #DRCongo #Wazalendo #StopM23 #MECAMEDIA

By mangwa