
🇷🇼🚨 RWANDA YAJIONDOA RASMI KUTOKA CEEAC KWA KULAUMU DRC
Malabo, 7 Juni 2025 – Serikali ya Rwanda imetangaza kujiondoa mara moja kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (CEEAC), kufuatia kile ilichokiita “ukiukaji wa wazi wa misingi ya jumuiya hiyo na upendeleo kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)”.
Katika taarifa rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Rwanda, Kigali inailaumu DRC kwa “kugeuza jumuiya kuwa chombo cha maslahi binafsi kwa msaada wa baadhi ya nchi wanachama”.
🔹 Kipengele kinachozua mgogoro:
Rwanda inadai kunyimwa kwa makusudi nafasi yake ya urais wa kupokezana (rotatif) katika mkutano wa 26 wa CEEAC uliofanyika 7 Juni 2025 huko Malabo, kinyume na Kifungu cha 6 cha mkataba wa CEEAC.
🔹 Rwanda yadokeza historia ya mvutano:
Kigali inakumbusha kuwa tayari mwaka 2023 ilishatoa malalamiko juu ya “kutengwa kinyume cha sheria” kwenye mkutano wa 22 uliofanyika Kinshasa, bila hatua yoyote kuchukuliwa na uongozi wa CEEAC au Umoja wa Afrika.
🔹 Kauli ya mwisho ya Rwanda:
“Tunaona hakuna tena sababu ya kuendelea kuwa mwanachama wa jumuiya ambayo haizingatii sheria zake wala kuheshimu usawa wa wanachama,” imesema taarifa hiyo.
Uamuzi huu wa Rwanda unakuja wakati uhusiano kati ya Kigali na Kinshasa ukiwa katika hali ya taharuki kubwa, hasa kufuatia mzozo unaoendelea mashariki mwa Kongo.
✍️ Imeandikwa na: MANGWA

